Mkutano mkuu wa mwaka ndio chombo kikuu kabisa katika mfumo wa ushirika. Kwa mujibu wa muongozo wa katiba katika vyama vya ushirika, kila mwaka ni lazima kuitisha mkutano mkuu kwaajili ya kujua mwenendo wa utekelezaji wa shughuli za chama. Mkutano mkuu unaudhuliwa na wajumbe wa bodi, Menejiment ambao ni Watendaji na wajumbe wengine ambao ni mwenyekiti, katibu na muwakilishi moja kutoka katika kila chama (AMCOS), Mrajisi msaidizi ni miongoni mwa waudhuliaji wa mkutano mkuu kwani ndio anamamlaka kisheria katika kuweka mizani sawa ya wanufaikaji/wakulima na watendaji wa chama. Hata hivyo mkutano mkuu unakuwa na wadau wengine waalikwa ambao wanafanya kazi na chama kama vile wakaguzi wa nje, Mwenyekiti, Katibu au mjumbe muwakilishi kutoka shirikisho la vyama vya ushirika, Viongozi mbali mbali wa serikali na wizara ya kilimo kulingana na waratibu watakavo ona inafaa na budgeti iliyopo.
Mkutano mkuu wa 13 wa mwaka wa chama kikuu cha ushirika cha mkoa wa mara (WAMACU) LTD uliofanyika katika ukumbi wa blue sky mjini tarime tarehe 19 januari 2023.