Ukaguzi wa Ndani

Ukaguzi wa ndani unafanywa na mtumishi alie ajiliwa na WAMACU LTD ili kuongeza ufanisi na utendaji wa shughuli za chama. Mkaguzi anawajibika kama ifuatavyo.

  • Kutekeleza na kuzingatia sharia ya vyama vya Ushiruka na kanuni zake, Sera ya maendeleo ya ushirika, Masharti ya chama, Kanuni na Sera mbalimbali zilizowekwa kwa ajili ya kuongeza utekelezaji na udhibiti wa ndani wa shughuli za chama
  • Kumsaidia mkuu wa idara ya msimamiaji wa fedha ya chama na kuwajibika kwa bodi na kwa MENEJA MKUU wa WAMACU LTD
  • Kusimamia sharia ya matumizi ya kanuni, Sera na masharti ya chama juu ya maswala yote ya uhasibu na fedha wa WAMACU LTD
  • Kusimamia maswala ya kiukaguzi wa fedha zote zinazopelekwa kwenye AMCOS zote ambazo ni wanachama wa WAMACU LTD
  • Kudhibiti matumizi mabovu ya fedha ya kahawa iliyopelekwa kwenye AMCOS wanachama wa UNION