Uhamasishaji na biashara ni jukumu la kila mtumishi likiongozwa na mwenyekiti wa bodi, Meneja Mkuu na mwanachama wa ushirika katika kutoa elimu na uelewa kwa wakulima wengine. Shughuli za uhamasishaji zinaweza zikafanyika kwa njia zifuatazo.
- Kuudhulia maonyesho mbali mbali kama vile maonyesho ya wakulima nane nane, maadhimisho ya siku ya ushirika duniani (SUD), Saba saba na ICUD
- Kushiriki katika shughuli mbali mbali za kijamii na Meneja kutoa salamu za chama
- Kutembelea vyama mbali mbali vya msingi na kuwahamasisha watie juhudi katika kilimo
- Upatikanaji wa pembejeo za kilimo kwa wakati na kumfikia mkulima
- Wakulima kupata malipo yao kwa wakati