MBOLEA

USAMBAZAJI NA MAUZO YA MBOLEA

Kwa msimu 2022/23  WAMACU LTD kwa kushirikiana na TFRA, pamoja na Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko (CPB) tumeweza kuagiza mbolea ya Ruzuku aina ya DAP na UREA na kuisambaza kwa wakulima wa Mkoa wa Mara na wilaya zake. Aidha WAMACU imefanya hivyo kwa ajili ya kuhakikisha inatatua changamoto ya upatikani wa mbolea kwa wakulima wetu ambao walikuwa wanalazimika kununua mbolea kutoka nchi jirani ya Kenya kwa gharama kubwa.

Mbolea hizi zinauzwa kwa bei elekezi ya serikali ya Tsh 70,000 kwa mfuko wa kilo 50 ambapo mkulima anahitajika kuja na namba yake ya siri aliyosajiliwa na Afisa kilimo pamoja na nakala ya kitambulisho cha nida au cha kura. Mbolea hizi tulizisambaza katika Wilaya tano za Mkoa wa Mara ambapo kwa Tarime mji zinapatikana kwenye maghala ya WAMACU Ltd yaliopo kanda maalumu, kwa Tarime DC inapatikana katika ghala la Chama cha Msingi cha Tagare, Rorya inapatikana katika ghala la Ryagoro mkabala na shule ya msingi Girango, Butiama inapitikana Buhemba na Bunda mjini kwenye ghala la Chama cha Msingi Bunda Stoo.

 

Jedwali 1.Mbolea zizosambazwa na kuuzwa katika wilaya za Mkoa wa Mara kwa msimu 2022/23

WILAYA DAP UREA UZWA(DAP) UZWA(UREA) BAKI(DAP) BAKI(UREA)
TARIME TC 1150 750 1090 750 0
TARIME DC 200 70 100 62 100 8
 RORYA 730 180 495 176 235 4
 BUTIAMA 200 50 7 50 193 0
 BUNDA 200 150 20 150 180
JUMLA 2480 1200 1775 1188 708 12