UZALISHAJI NA UGAWAJI WA MICHE
Chama kinaendelea kusubiria kupokea fedha ya mkopo wa miche uliosalia kutoka Benki ya kilimo (TADB) kwa ajili ya kuendelea na uzalishaji wa miche vitaluni. Aidha fedha iliyotolewa kwenda TaCRI ni milioni tisini na tisa (99,000,000/=) kwa ajili ya kujenga vitalu vinne vya kuzalisha miche. Kama chama kitafanikiwa kuwekewa fedha hiyo kitaendelea na zoezi hilo maana kwa sasa hatuhitaji kujenga vitalu zaidi ya tulivyonavyo.