MAKUSANYO KWA MSIMU

UKUSANYAJI WA KAHAWA

Katika Msimu wa 2022/2023 Chama kimekusanya kahawa kutoka kwenye Vyama wanachama wa Itiryo, Kema, Goronga, Tagare, Bungurere, Kangarian, Muriba, Kemakorere, Mbogi, Nyakonga, Nyandurumo, Nyamwigoma, Nkongore, Mwesu, Sirari, Nyantira, Mori,Mogabiri Shadabi pamoja na Taasisi ya JKT Ng’ereng’ere kupitia Mwesu. Katika jedwali hili tumeainisha makusanyo ya kahawa ya maganda ki-wilaya kwa Msimu 2021-22, 2021-22 na 2022-23 kama inavyoonekana hapa chini: –

Jedwali Na. 1 Ukusanyaji wa Kahawa kwa Misimu Mitatu kuanzia 2020 mpka 2023

                               KAHAWA YA MAGANDA ILIYOKUSANYWA
WILAYA 2020-2021 2021-2022 2022-23
TARIME DC           268,704 165,450 232,248
TARIME TC               3,429 6,031      6,740
BUCHOSA             10,384 7,192
BUTIAMA 1,468
 JUMLA          282,517 171,481                  247,648

Aidha Chama katika Msimu huu kilianza kukusanya kahawa kwa bei yaTZS.1600/=, kupitia Mkutano Mkuu Maalum wa tarehe 30/05/2022 uliazimia kuongeza bei na kufikia TZS.2,200/= na baadaye Bodi iliongeza hadi kufikia TZS. 2400/= ambayo ndiyo imekuwa bei ya Msimu wa 2022/2023. Pia kwa msimu huu Vyama vyote vimekusanya kahawa yao kupitia WAMACU LTD. Hata hivyo kwa sasa tunachangamoto ya kupata kahawa kutoka JKT Ng’ereng’ere pamoja na kuwa wametupa gunia 11 kupitia MWESU amcos.

 

  • MAUZO YA KAHAWA

Kwa msimu 2022/23 WAMACU LTD imeuza kahawa yake katika mnada wa Bukoba kiasi cha kg. 125,203 ambazo ni kahawa kavu ya maganda aina ya Arabica. kwa misimu huu imetulazimu kuuza kahawa ya maganda kutokana na kiwanda ambacho awali tulikuwa tunatumia kuchakata kahawa ya wakulima kuongolewa na mmiliki wake ambae ni AMRI HAMZA (T) LTD.Hata hivyo tulijitahidi kuwasiliana na Nothern highland ili tuweze kukobolea kahawa yetu katika kiwanda chao lakini ilishindikana kutokana na gharama kuwa kubwa ukilinganishana malipo ya Tsh 225 ambayo tulikuwa tunalipa kwa kahawa safi huku wao wakitaka tuwalipe kwa kahawa ya maganda kwa Tsh 220 kwa kila kilo ya kahawa kavu ya maganda.katika kutatua changomoto hii,tayari tumeagiza mashine mbili ya kuchakata kahawa kavu na kahawa mbivu na tayari mwakilishi wa kampuni ya JM ESTRADA alifika ofisini kwetu na kukutana na wajumbe pamoja na kupima maeneo ambayo mashine hizo zinatarajiwa kusimikwa mwezi ujao.

Jedwali Na. Mauzo ya kahawa kavu ya maganda Kwa kila Wilaya

WILAYA KAHAWA ILIYOUZWA(KG) BEI (TSH 4000@KG) KAHAWA ILIYOBAKI (KG)
TARIME DC 115,055 460,220,00 117,193
TARIME TC 5,593 22,372,000 1147
BUCHOSA 3,858 15,432,000 3,334
SHADABI 697 2,788,000 771
JUMLA 125,203                  500,081,200 122,445