Baada ya kupata watumishi wenye sifa stahiki tutaendelea kushirikiana na taasisi zinazo jishughulisha na kilimo na masoko ya kahawa kwaajili ya kuimarisha uzalishaji wa kahawa. TaCRI imekuwa mdau mkubwa wa biashara yetu katika kupanua wigo wa uzalishaji wa miche kwaajili ya wakulima wetu.
Hivyo basi chama kinaendeleza jitihada za kukuza miche mingi Zaidi kwa kupitia vikundi vilivyo chini ya TaCRI na TaCRI yenyewe kwaajili ya kuhakikisha upatikanaji wa miche ya kahawa unaongezeka kutoka hapa tulipo sasa.
YAFUATAYO NI BAADHI YA MAJUKUMU YA MAAFISA KILIMO WA WAMACU
- Kushirikiana na wakulima kuendesha mashamba darasa katika wanaushirka
- Kushauri wanachama na wakulima matumizi bora ya mbolea inayosambazwa na UNION.
- Kuhakikisha kuwa wakulima wote wanaokuja ghalani kununua mbolea wanapatiwa msaada wa kitaalamu ( ushauri) juu ya matumizi bora ya mbolea, mbegu na viuatilifu
- Kutembelea wakulima/vikundi vya wakulima katika mashamba yao na kutoa ushauri wa kitaalamu juu ya mbinu bora na za kisasa za kilimo cha biashara.
- Kukusanya na kuunza taarifa za hali ya kilimo katika vyaama wanachama wa UNION.
- Kubuni na kuandaa, na kuwafundisha wakulima ujenzi wa vihengo bora vya kisasa vya kuhifadhi mazao na kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mazao.
- Kutoa taarifa juu ya dalili za kuwepo visumbufu vya mimea/ mazao kwa wanachama
- Kuandaa na kutumia daftari la kilimo katika kutekeleza majukumu ya kazi za kila siku
- Kushiriki katika mchakato wa kuibua fursa na vikwazo vya maendeleo ya wanachama na kuandaa mpango wa maendeleo ya kilimo ya wanachama wa AMCOS zote za UNION.
- Kuandaa taarifa ya utekelezaji ya kila mwezi na kuiwasilisha kwa MENEJA MKUU wa UNION.
- Kusimamia shughuli za kilimo za WAMACU LTD, AMCOS na wanachama wake kulingana na sheria ya ushirika,masharti, kanuni na sera za kilimo.
- Kufuatilia miche yote iliyopelekwa kwenye AMCOS na kubainisha wakulima waliokopeshwa kwa ajili ya kurudisha fedha waliokopeshwa
- Kuhakikisha kuwa taarifa zote za pembejeo za kilimo zinarekodiwana kutunzwa kwa usahihi ili kuimarisha udhibiti wa ndani.
- Kutekeleza majukumu mengine yote kadri utakavyopangiwa na MENEJA MKUU wa WAMACU LTD.
- Kuandaa programe za mafunzo kwa wakulima kutumia zana bora za kilimo
- Kuwafundisha wakulima matumizi bora ya kilimo cha umwagiliaji.