KAHAWA

MUHTASARI WA MAKISIO YA MSIMU WA 2023/2024

kwa Msimu 2023/2024 tunatarajia kukusanya kilo 1,023,100 za Kahawa kavu za maganda na kilo 2,215,500 za Kahawa mbivu ambazo tutalipa Tsh 5,114,040,000 kama malipo ya awali kwa Mkulima (tazama KA1 kwenye makisio). Pia tunatarajia kupata mauzo ya Tsh 6,622,325,000 ya Kahawa safi inayotokana na kilo 800,727 ya daraja la kwanza na kilo 167,771 ya chenga (tazama uk Na. 00).

  • MAUZO YA KAHAWA

Kwa msimu 2022/23 WAMACU LTD imeuza kahawa yake katika mnada wa Bukoba kiasi cha kg. 125,203 ambazo ni kahawa kavu ya maganda aina ya Arabica. kwa misimu huu imetulazimu kuuza kahawa ya maganda kutokana na kiwanda ambacho awali tulikuwa tunatumia kuchakata kahawa ya wakulima kuongolewa na mmiliki wake ambae ni AMRI HAMZA (T) LTD.Hata hivyo tulijitahidi kuwasiliana na Nothern highland ili tuweze kukobolea kahawa yetu katika kiwanda chao lakini ilishindikana kutokana na gharama kuwa kubwa ukilinganishana malipo ya Tsh 225 ambayo tulikuwa tunalipa kwa kahawa safi huku wao wakitaka tuwalipe kwa kahawa ya maganda kwa Tsh 220 kwa kila kilo ya kahawa kavu ya maganda.katika kutatua changomoto hii,tayari tumeagiza mashine mbili ya kuchakata kahawa kavu na kahawa mbivu na tayari mwakilishi wa kampuni ya JM ESTRADA alifika ofisini kwetu na kukutana na wajumbe pamoja na kupima maeneo ambayo mashine hizo zinatarajiwa kusimikwa mwezi ujao.

Jedwali Na. Mauzo ya kahawa kavu ya maganda Kwa kila Wilaya

WILAYA KAHAWA ILIYOUZWA(KG) BEI (TSH 4000@KG) KAHAWA ILIYOBAKI (KG)
TARIME DC 115,055 460,220,00 117,193
TARIME TC 5,593 22,372,000 1147
BUCHOSA 3,858 15,432,000 3,334
SHADABI 697 2,788,000 771
JUMLA 125,203                  500,081,200 122,445

 

MAPATO KWA MSIMU 2022/2023

Muhtasari wa Mapato.

Chama kime-endelea kutegemea kwa kiasi kikubwa mkopo kutoka Benki ya Kilimo TADB kwa matumizi ya kawaida na matumizi ya mtaji. Katika msimu 2022/2023 chama kimefanikiwa kupata jumla ya mapato kama yanavyoonekana hapo juu. Aidha mapato hayo yanategemewa kuongezeka zaidi baada ya kuwa tumeuza kilo  zaidi ya Kg 122,445 zilizopo ghalani hadi kufikia March, 2023.