Mamlaka Wajibu na Kazi

WAMACU kama chama cha ushirika kilichoidhinishwa na kufuata taratibu zote za usajiri na kupata hati ya usajiri ya nambari 5573 kina mamlaka ya kufanya shughuli mbalimbali zinazo husiana na kilimo ikishirikiana na tume ya maendeleo ya ushirika pamoja na wizara ya kilimo.

WAJIBU NA KAZI

Wajibu wa chama cha wakulima wa mara cooperative union (WAMACU) kulingana na kanuni na taratibu ya vyama vya ushirika nnchini ni kama ifuatavyo.

  • Ukusanyaji wa kahawa ya mkulima kutoka vyama vya msingi
  • Uchakataji wa kahawa ya maganda
  • Utafutaji wa masoko ya kahawa ndani nan je ya nchi
  • Kukopesha miche na pembejeo kwa wakulima wa kahawa
  • Kusambaza mbolea aina ya DAP, UREA, NPS na NPK katika wilaya zote za mkoa wa Mara.
  • Kutoa huduma kwa wakulima wa tumbaku wilayani Serengeti kuanzia msimu 2023/24
  • Kusambaza pembejeo za kilimo kama vile mbegu za mazao mbalimbali kwa msimu 2023/24