Mwenyekiti wa Bodi

MOMANYI RANGE

Karibu

Karibu Chama Kikuu cha Ushirika cha Wakulima wa Mkoa wa Mara (WAMACU) LTD, ninayo furaha kukukaribisha kwenye Tovuti ya WAMACU. Hapa utaweza kupata kujua kazi zetu, muundo wa taasisi yetu, Viongozi na mengi kuhusu chama.

Shughuli zetu za kununua Kahawa, kusafirisha, kusimamia, kueneza elimu ya ushirika kwa wakulima, vyama vya ushirika, wanachama, bodi za vyama vya ushirika na watumishi wake.

Chama kinafanya shughulika zake ndani ya Mkoa wa Mara.

Karibuni kutembelea Tovuti yetu na kujua imani yetu juu ya Chama na Wanachama.

Furahiya…

CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA CHA WAKULIMA WA MKOA WA MARA (WAMACU) LTD kilisajiliwa chini ya sheria Namba 20 ya Vyama vya Ushirika ya mwaka 2003. Chama kiliandikishwa rasmi katika daftari la Mrajis wa vyama vya Ushirika tarehe 24 Desemba, 2008 nakupewa Hati ya usajili yenye Namba 5573.

Malengo ya msingi ya ushirika yanayojumuisha madhumuni ya Chama Kikuu cha Ushirika katika kuinua na kusitawisha hali ya uchumi na maisha ya wanachama kwa ujumla wake, kwa kufuata misingi ya demokrasio ya kweli, sheria, kanuni na taratibu za Tume ya Maendeleo ya ushirika kwa mujibu wa sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 6 ya mwaka 2013.

MAFANIKIO

Yafuatayo ni baadhi ya mafanikio yaliyopatikana kupitia Chama Kikuu cha Ushirika wa Wakulima wa Mara:

  • Kukabidhiwa mali: Chama kimeweza kukabidhiwa kwa zilizokuwa Mali za EX-MCU (1984) Ltd na kurejeshwa kwa mali za ushirika katika kata ya Matongo, kijiji cha Nyangoto ambazo ni eneo la ghala (kiwanja namba 435 na 436) na Kasiki.

  • Kusambaza mbolea: Chama kimefanikiwa kuwasambazia wakulima Mbolea ya Ruzuku kwa kushirikiana na TFRA na CPB

  • Kuajiri  watumishi  wenye  weledi:  Chama kwa sasa kina watumishi wenye weledi wa kutosha wa kuwahudumia wakulima na wadau wengine wa biashara bila shida.

  • Kukusanya kahawa kwa fedha Taslimu: Chama kimeendelea na utaratibu wa ukusanyaji wa mazao kwa fedha taslimu jambo ambalo wakulima nao wamelipenda na wanapongeza na  kushauri  tuendelee na mfumo huu katika kuimarisha Ushirika na kuongeza makusanyo.

  • Kukusanya kahawa kwa malipo ya kwanza TZS.2400: katika msimu huu hii bei nayo imekuwa ni mafanikio makubwa wakulima maana imeleta changamoto kubwa sana kwa wanunuzi binafsi na kupelekea mkulima kunufaika katika kuuza kwa bei nzuri, kwetu hiyo ni mafanikio makubwa sana.

  • Malipo ya pili kwa Mkulima: Chama kwa kwa Msimu wa 2020/2021 kilifanikiwa kumlipa mkulima malipo ya pili yenye TZS.400/kilo, jambo ambalo limeongeza tija na hamasa kwa wakulima wetu wa kahawa katika Mkoa mzima. Na hii ilituwezesha kulipa kutumia jumla ya 113, 006,800/=

  • Kupata mkopo wa mashine za kuchakata kahawa: Chama kimefanikiwa kupata mkopo wa  mashine  za  kuchakata  kahawa  kavu wa  kiwanda  cha kuchakata  kahawa  tayari umeshaanza

UJENZI WA KIWANDA CHAKUCHAKATA KAHAWA